Skip to main content

Marekani yaitaka Russia kuheshimu haki za Wamarekani waliotekwa Ukraine

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema Mmarekani wa tatu anaaminika kutoweka nchini Ukraine mbali na wanajeshi hao wawili waliostaafu ambao waliripotiwa kutekwa na wanajeshi wa Russia katika mapambano makali wiki iliyopita.

“Warussia wana wajibu fulani na wanajeshi wa Ukraine ikiwemo wapiganaji wanaojitolea ambao wanaweza kuwa raia wa nchi nyingine waliojumuishwa katika jeshi wanapaswa kuchukuliwa kama wafungwa wa vita chini ya mikataba ya Geneva,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ned Price aliwambia waandishi wa habari.

Wafungwa wa vita lazima wapewe huduma na ulinzi unaolingana na hadhi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa kiubinadamu na kuheshimu haki zao za kimsingi za kujitetea mahakamani,” alisema.

Familia na wabunge wa Marekani Jumatano walisema Alexander Drueke na Andy Huynh, wote wakiwa wanajeshi wa Marekani waliostafu ambao walikuwa wanaishi Alabama, walipoteza mawasiliano na jamaa zao wiki iliyopita wakipigana upande wa wanajeshi wa Ukraine karibu na mpaka wa Russia.

The post Marekani yaitaka Russia kuheshimu haki za Wamarekani waliotekwa Ukraine appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/25154/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT