Skip to main content

Mamia waandamana kupinga mabadiliko ya katiba Tunisia

Waandamanaji mjini Tunis wameitikia wito wa makundi ya upinzani, ikiwemo chama hasimu cha Saied cha kiislamu cha Ennahdha, wakiimba “katiba, uhuru, na utu”, na “wananchi wanataka mahakama huru”, mwandishi wa habari wa AFP amesema.

Katiba mpya ni sehemu ya mipango ya mageuzi ya Saied na itarajiwa kupelekwa kwenye kura ya maoni tarehe 25 Julai, mwaka mmoja baada ya kuifuta kazi serikali na kulisimamisha bunge.

Tangu wakati huo alijiongezea mamlaka, ikiwemo kulivunja bunge mwezi Machi.

Mapema mwezi huu, aliwafuta kazi majaji 57, baada ya kuwashtumu wengi kula rushwa na uhalifu mwingine.

“Kura ya maoni sio kitu kingine isipokuwa udanganyifu,”, amesema Ali Layaredh, kiongozi kutoka chama cha Ennahdha, ambacho kilikuwa chama kikuu katika bunge na katika serikali iliyofutwa kazi na rais.

“Tunaandamana dhidi ya kuitenga mamlaka ya mahakama na dhidi ya mapinduzi ambayo yanailenga katiba,” amesema.

The post Mamia waandamana kupinga mabadiliko ya katiba Tunisia appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/25905/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT