Skip to main content

Felicien Kabuga, mshukiwa mkuu katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda yuko tayari kiafya kujibu mashtaka dhidi yake: Mahakama ya UN

“Upande wa utetezi haujathibitisha kwamba Kabuga kwa sasa hawezi kwendelea na kesi kwa sababu ya afya yake,” uamuzi huo wa mahakama umesema, baada ya mawakili wake kutaka kesi hiyo isimamishwe kwa misingi ya kiafya.

Kabuga alikamatwa tarehe 16 Mei mwaka wa 2020 katika kitongoji kimoja mjini Paris, baada ya kukaa mafichoni kwa miaka 25.
Anashutumiwa kusaidia kuunda kundi la wanamgambo wa Interahamwe, kundi kuu lenye silaha ambalo lilihusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 800,000 kulingana na Umoja wa mataifa.

Kabuga, mwenye umri wa miaka 87, yuko jela kwa sasa mjini The Hague, Uholanzi, akisubiri kufikishwa mbele ya mahakama maalum ya kimataifa ya uhalifu (MICT), ambayo inakamilisha kazi ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya Rwanda, iliyovunjwa.

Wataalamu mbalimbali walihusika katika kuandaa shauri hilo, ambalo linadhihirisha bila shaka kwamba Kabuga yuko katika hali ya hatari na dhaifu na anahitaji huduma ya matibabu na ufuatiliaji wa kina, mahakama hiyo MICT ilisema.

The post Felicien Kabuga, mshukiwa mkuu katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda yuko tayari kiafya kujibu mashtaka dhidi yake: Mahakama ya UN appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/24045/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT