Skip to main content

Faidika Microfinance Tanzania yaja kivingine

*Zaidi ya Sh bilioni 20 kukopeshwa wafanyabiashara wa kati na wadogo

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Taasisi ya kifedha ya Faidika Microfinance Tanzania imetenga zaidi ya Sh Bilioni 20 kwa ajili ya kukopesha wafanyabiashara wadogo na wa kati kupitia program yao ijulikanayo kwa jina la “MKOPO FASTA”.

Akizungumza juzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Faidika Microfinance Tanzania, Baraka Munisi amesema kuwa mkopo huo utolewa kwa muda mfupi na masharti nafuu na kuwaomba wafanyabishara wachangamikie kukopa.

Munisi alisema kuwa sababu ya Faidika Microfinance kutoa mkopo huo ni kuwainua vipato wafanyabishara ili kuwawezesha kupata maendeleo kama kauli mbiu yao ya ‘’Lets Improve Life’’ inavyosema.

“Tunajua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wafanyabisahara wadogo na wa kati, hivyo tumeamua kuleta mpango huu maalum wa kuwasaidia kuzikabili changamoto hizo.

“Hivyo ili mfanyabiashara aweze kupata mkopo, anahitaji kuwa na leseni ya biashara, namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) na cheti kilichohidhinishwa cha ushuru, picha, kitambu-lisho cha serikali kinachotambulika.

“Miezi kadhaa iliyopita Faidika ilizindua programu ya “LetsGO Digital Mall” ambayo unamwezesha mteja wao kupata huduma bora kwa njia rahisi na haraka zaidi. Kupitia LetsGo Digital Mall, mteja anaweza kujihudumia wenyewe kutoka kiganjani mwa simu yake. Tunaamini njia hii itarahisisha mteja kupata mkopo wa kibiashara kwa urahisi zaidi,” amesema Munisi.

Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Mauzo, Masoko na Mifumo wa Faidika Microfinance Tanzania, Asupya Bussi Nalingigwa alisema kuwa wamejipanga kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wao na kuwaomba kuanza kuwasilisha maombi.

Nalingigwa amesema kuwa taasisi yao inajivunia kutoa huduma bora za kifedha na jambo zuri zaidi ni kuwa na matawi mengi ya kutoa huduma hiyo hapa nchini.

“Ni fursa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na wakati kupata mkopo kutoka taasisi yetu, tena wenye mashari nafuu na kwa njia ya haraka zaidi. Tunawakaribisha ili kuweza kuinua biashara zao na vilevile kipato,” hapa kwetu mambo yote ‘’MKOPO FASTA’,” amesema Nalingigwa.

Alifafanua kuwa ili kuweza kuwafikia wateja wengi taasisi yao imeanzisha namba maalum ambapo mteja anatakiwa kutuma neno FAIDIKA kwenda namba 15062 kisha kuchagua ‘’1’’ na kuanza kupata huduma kutoka kwa maofisa wao.

The post Faidika Microfinance Tanzania yaja kivingine appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/24034/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT