Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene ameongoza kikao cha Mawaziri kwa lengo la kujadil…

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene ameongoza kikao cha Mawaziri kwa lengo la kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za makazi.
Kikao hicho kimefanyika leo Mei 27, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma ambapo kilihudhuriwa na mawaziri mbalimbali wakiwemo Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Hamza Hassan Juma, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula.
Aidha kikao hicho kimefanyika kama sehemu ya maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 2022 nchini ambapo itakuwa Sensa ya sita tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, Ambapo hufanyika kila baada ya miaka 10.
#StarTvUpdates

The post Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene ameongoza kikao cha Mawaziri kwa lengo la kujadil… appeared first on soka letu.
source https://mjombazecoder.website/19275/
Comments
Post a Comment