Skip to main content

Taarifa za mfumo wa anwani za makazi kutumika kwenye mawasiliano

Na Mwandishi Wetu, Pwani

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya ameshauri Watendaji kuanza kutumia taarifa za mfumo wa Anwani za makazi Postikodi kwenye barua za ofisi ili kurahisha mawasiliano kwa watu kujua eneo zinapopatikana Ofisi.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya akizungumza na Watendaji (hawapo pichani) katika Ofisi ya Mtendaji, Kata Matumbi kukagua utekelezaji wa operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya Mji wa Kibaha.

Naibu Katibu Mkuu huyo ameyasma hayo leo Alhamisi Mei 19, 2022 katika ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Kibaha Mji, mkoani Pwani alipofika kujionea utekelezaji wa Operesheni Anwani za makazi.

“Watendaji tuanze kujitambulisha kwenye mikutano kwa mfumo wa Anwani za makazi ili kutoa hamasa zaidi kwa wananchi,” amesema Mmuya.

Upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mkoani A Kibaha, Jakson Mwakalima amesema tayari wameshapata mtengenezaji wa vibao vya nyumba, ambavyo mwananchi anaenda kununua kwa shilingi elfu Mbili na kubandika kwenye nyumba yake.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mji, mara baada ya kukagua utekelezaji wa Operesheni Anwani za Makazi katika Halmashauri ya Mji huo.
 

The post Taarifa za mfumo wa anwani za makazi kutumika kwenye mawasiliano appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/UFgRaWi

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT