Skip to main content

Serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya Vyuo vya Ufundi

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Serikali imesema itaendelea kutoa fedha za kuboresha miundombinu ya Vyuo vya Ufundi ili wanafunzi wa Kitanzania waendelee kupata elimu katika mazingira bora.

Hayo yamesemwa leo Mei 24, 2022 Jijini Arusha na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (Mb) wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la maabara, madarasa na ofisi (Ufundi Tower) katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).

Amesema Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha sekta ya Elimu kuanzia Awali hadi Vyuo Vikuu kwa wanafunzi wa kawaida na wenye mahitaji maalum.

“Tumejenga madarasa, mabweni, maabara za masomo ya sayansi, tumeongeza nyumba za walimu, majiko na mabwalo ili watoto wa Kitanzania waweze kupata elimu bora bila changamoto yoyote,” amesema Majaliwa.

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa Serikali pia inafanyia kazi suala la upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa ngazi ya Diploma kupitia tume ya kutathmini iliyoundwa na Wizara ya Elimu ili kuona namna ya kuweza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ngazi ya kati.

“Kupitia bajeti ya mwaka huu ambayo inafikia bilioni 570 tunataka tuone kila mwanafunzi wa Kitanzania anayetoka kwenye familia isiyokuwa na uwezo wa kujilipia gharama mbalimbali ananufaika na mkopo huo,” amefafanuaMajaliwa.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo akiongea katika hafla hiyo kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb) amesema Wizara ilipokea jumla ya Sh bilioni 64.9 kutoka kwenye fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19 ambazo zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kielimu.

“Mradi huu ulioweka jiwe la msingi leo ni matokeo ya jitihada kubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita lakini pia na ushawishi mkubwa wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuweza kupata fedha hizo ili kuweza kukamilisha miradi hii,” amesema Prof. Nombo.

Ameongeza kuwa pamoja na kuwa Uviko imekuwa ni changamoto lakini kwa Tanzania imekuwa ni baraka pia kwa kuwa fedha zake zimeweza kutumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia.

“Fedha hizi zimeelekezwa katika Vyuo vya VETA 25 vya Wilaya, vinne vya mikoa, Vyuo vya Ualimu ambako tumejenga madarasa, mabweni na kumbi la mihadhara kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia,” amefafanua Prof. Nombo.

Naye Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt Musa Chacha amesema ujenzi wa jengo la ufundi tower ulianza Januari 2022 na unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi Juni 2022.

“Jengo hili lina ghorofa tatu na litakuwa na maabara, madarasa, ofisi na stoo na ujenzi wake mpaka sasa umefikia asilimia 88,” amesema Dk. Chacha.

The post Serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya Vyuo vya Ufundi appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/18551/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT