Skip to main content

Kampuni ya Nestle itasafirisha maziwa ya watoto kutoka Uswizi na Uholanzi kwenda Marekani

Kampuni kubwa ya chakula ya Uswizi ya Nestle itasafirisha maziwa ya watoto kutoka uswizi na Uholanzi hadi Marekani kufuatia uhaba wa maziwa uliopo msemaji wa kundi hilo alisema Jumanne.

Kampuni ya Uswizi itaingiza chapa mbili za maziwa yasiyo na athari za mzio kutokana na uhaba huo ambao umekuwa chanzo cha ziada cha msongo wa mawazo kwa wazazi wenye watoto wadogo wasiostahimili protini za maziwa ya ng’ombe.

“Tulizipa kipaumbele bidhaa hizi kwa sababu zinatumika kwa madhumuni muhimu ya matibabu” msemaji huyo aliliambia shirika la habari la AFP akithibitisha ripoti za vyombo vya habari.

Bidhaa hizi mbili tayari zimeagizwa kutoka nje; maziwa ya Gerber Good Start Extensive HA kutoka Uholanzi na maziwa ya Alfamino kutoka Uswizi. Ikikabiliwa na uhaba huo Nestle iliamua kusafirisha maziwa hayo kwa ndege ili kusaidia kukidhi mahitaji ya haraka lilisema kundi hilo ambalo pia lina viwanda viwili nchini Marekani vinavyozalisha maziwa ya watoto wachanga.

The post Kampuni ya Nestle itasafirisha maziwa ya watoto kutoka Uswizi na Uholanzi kwenda Marekani appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/XYWwbU4

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT