Skip to main content

Halotel yazindua ‘Toboa na Halotel 4G’

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya Halotel Tanzania imeendelea kuwahakikishia wateja ubora na kasi ya mtandao wake kwa kuwapa huduma zenye ubunifu na kuendelea kuboresha huduma za mawasiliano hapa nchini.

Wakati ikifanya jitihada hizo, Halotel pia imekuwa ikibuni bidhaa mpya zenye lengo la kuwazawadia wateja wake wanaotumia huduma za mtandao.

Mkurugenzi wa Biashara cha Halotel, Abdallah Salum amesema: “Leo kampuni ina habari njema kwa wateja wetu: tunazindua kampeni mpya ya mtandao wa 4G. Kampeni hiyo inaitwa ‘Toboa na Halotel 4G.’

Kampeni hii itawapa fursa wateja kushiriki katika promosheni hii itakayoendeshwa kwa wiki 8 ambapo washindi watapata zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu na simu janja.

Ili kushiriki katika promosheni hii ya Toboa na Halotel 4G, wateja ambao wanatumia 3G wanaweza kubadili laini kwenda 4G bila gharama yoyote au  mteja anaweza kusajili laini ya 4G na kuanza kutumia vifurushi vya intaneti kwa gharama nafuu na moja kwa moja atakuwa katika nafasi ya kuingia kwenye droo ya bahati na kuweza kuibuka mshindi.

Pia mteja anapaswa awe ameshatumia angalau 100MB ndani ya siku tatu kuanzia siku aliyoanza kutumia mtandao wa 4G.

Kampuni itawazawadia washindi 10 kila siku, kila mmoja atapata fedha taslimu kiasi cha Sh 100,000.

“Kila wiki washindi watatu (03) watazawadiwa simu janja ambapo mshindi wa kwanza atapata IPhone 13 pro max, mshindi wa pili atapata Samsung galaxy S22, na mshindi wa tatu atapata Samsung Galaxy A72,” amesema Salum.

Kampuni imezindua kampeni hii kwa kuzingatia kwamba tayari mtandao wake wa 4G umeenea katika maeneo mengi ambapo kwa sasa ina vituo vipatavyo 1037 vinavyosambaza mtandao wa 4G, hivyo mtandao wa 4G umeongeza nguvu na ufikiaji wa maeneo mengi ya nchi.

Sababu zingine za kuanzisha kampeni hii ni kuwapa wateja uzoefu juu ya ubora wa 4G huku ikiwapitia zawadi mbalimbali, na hivyo kufanya huduma hiyo kuwafikia Watanzania wengi zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa sasa mtandao wa 4G umewafikia asilimia 45 ya Watanzania.    

“Hii ni kutokana na kukua kwa huduma za kidijitali hapa Tanzania na kuongezeka kwa uhitaji katika soko, na hivyo uwekezaji mkubwa wa kampuni umeelekezwa kwenye miundombinu katika juhudi za kuongeza vituo vya usambazaji mtandao wa 4G,” amesema Salum.

Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel, Abdallah Salum akiongea na waandishi wa Habari katika ofisi za makao makuu ya Halotel leo wakati wa uzinduzi rasmi wa Promosheni mpya inayojulikana kwa jina la “Toboa na Halotel 4G” inayowapa wateja wote wa Halotel walioko mjini na vijijini fursa ya kujishindia zawadi za Fedha Taslimu kila siku pamoja na Simu Kajanja Mpya kabisa ikiwemo iPhone 13 Promax maarufu kama “Macho Matatu” kila wiki. Mteja anapaswa kubadili laini yake ya 3G kuwa 4G au kusajili Laini mpya ya 4G na kutumia intaneti ili kuweza kupata fursa ya kuingia kwenye droo ya kuwa mshindi. Promeshini hii itaendeshwa kwa muda wa wiki nane (8) ni maalumu kwa wateja wa Halotel.

Ameongeza kuwa katika maeneo ambayo yana mtandao wa 2G kampuni itaboresha na kuwa 3G na maeneo yenye 3G watapata 4G.

Halotel itawekeza zaidi kuongeza ubora wa mtandao Kwa sababu Watanzania milioni 29.8, au karibu nusu ya Watanzania wanatumia huduma za intaneti, tafiti mpya inaonesha kuwa Halotel ina mtandao wenye kasi zaidi kuliko mitandao yote hapa nchini.

Kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita kampuni imekuwa ikijielekeza katika mikakati ya kupanua wigo wa mtandao wake hapa Tanzania.

Kwa kuzingatia kuwa asilimia 30 ya wateja wake wanatumia mtandao wa intaneti, kampuni inapanga kuongeza idadi hiyo kufikia asilimia 40 ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Halotel tayari imeanza kuzindua kizazi cha nne cha huduma za mtandao wa 4G katika maeneo mengi ya nchi.

The post Halotel yazindua ‘Toboa na Halotel 4G’ appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/UFgRaWi

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT