
Taarifa hiyo ya Bintou Keita, mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa inajiri baada ya jeshi la DRC kuanzisha mashambulizi dhidi ya kundi la M23 siku ya Alhamisi.
Taarifa ya Keita imelaani shambulio la kundi hilo dhidi ya wanajeshi wa serikali na kikosi cha walinda amani wa MONUSCO.
“Waasi wa M23 walilenga kwa makusudi walinda amani wa Monusco ambao walijibu kwa risasi, kulingana na mamlaka yao,” Keita amesema.
Jeshi la DRC na wanajeshi wa Monusco walianzisha operesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa M23, taarifa ya Keita imeongeza.

The post DRC: Kundi la waasi la M23 lashtumiwa kushambulia walinda amani wa Umoja wa mataifa appeared first on soka letu.
Via soka letu https://ift.tt/zMfCiAI
Comments
Post a Comment