Skip to main content

Apple Music yasherehekea mafanikio ya Bara la Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

JUKWAA la muziki la Apple Music, linasherehekea uzuri wa kipekee na mandhari ya Bara la Afrika kupitia muziki katika Africa Month (Mwezi wa Afrika) unaokwenda sambamba na kampeni maalum ya Africa Is… yenye lengo la kuuenzi na kuutangaza ubunifu na vipaji vya muziki vya Kiafrika.

Kampeni ya Africa Is… itawashirikisha mastaa kibao wa muziki kutoka nchi za Afrika Mashariki, Magharibi, Kati na Kusini ambapo wasanii wakubwa takribani 18 wataonesha maana halisi ya kuwa Mwafrika.

Miongoni mwa wasanii watakaoshiriki kwenye kampeni hiyo kutioka Afrika Magharibi ni pamoja na Rema (Nigeria), Moliy (Ghana) Basketmouth (Nigeria) Kelvyn Boy (Ghana), Prince Gyasi (Ghana) na Andrea Iyamah (Nigeria).

Kwa upande wa Afrika Mashariki, wasanii watakaoshiriki kampeni hiyo ni pamoja na Chimano (Kenya) na Hussein Suleiman (Uganda) huku nchi zinazozungumza Kireno zikiwakilishwa na Soraia Ramos (Cape Verde) na Eliana Murargy wa Msumbiji.

Nchi zinazozungumza Kifaransa zitawakilishwa na Ferre Gola (DRC), Serge Ibaka (DRC) na Chrystel (Ivory Coast) na upande wa Afrika Kusini ikiwakilishwa na Bongeziwe Mabandla, Uncle Waffles, Slikour, Nduduzo Makhathini na Wanda Lephoto.

Pia Apple Music watakuwa na vipengele vingine kama playlist za Editorial, Genre, Artist Essentials na Behind The Boards pamoja na Exclusive Home Sessions.

“Kwangu mimi, Afrika, kama ulivyo muziki wetu, ni tajiri, wenye rangi za kuvutia na mandhari nzuri. Tunajua namna ya kufurahi. Tunajua namna ya kuleta mwangaza wa burudani kwenye chumba chenye giza, huku tukiutunza utu wetu na muziki wetu.

“Najua kampeni hii haitoshi kuwakilisha muziki wote wa Afrika lakini ni kitu kikubwa sana,” alisema Rema, ambaye ni miongoni mwa washiriki kutoka Nigeria.

http://music.apple.com/

The post Apple Music yasherehekea mafanikio ya Bara la Afrika appeared first on soka letu.

Via soka letu https://ift.tt/zjVpUe2

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT