Skip to main content

Wakati Mataifa mbalimbali duniani yakiingia kwenye changamoto ya upatikanaji wa nishati ya mafuta na mfumuko wa Bei wa nishati h…

Wakati Mataifa mbalimbali duniani yakiingia kwenye changamoto ya upatikanaji wa nishati ya mafuta na mfumuko wa Bei wa nishati hiyo inayotokana na Vita kati ya Urusi na Ukraine, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Ewura imeeleza kuwa bado Tanzania haijafikia kwenye hali Mbaya ya upatikanaji wa Mafuta.

Akizungumza katika Kikao kazi cha Mamlaka hiyo na Wahariri wa Vyombo vya Habari Jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Ewura Mhandisi Godfrey Chibulunje amesema kwasasa Tanzania ina Hifadhi ya mafuta ya petrol yanayoweza kutumika kwa siku 28 nchini bila kuingiza mengine, wakati Hifadhi ya Diesel imebaki ya siku 19 huku Hifadhi ya mafuta ya Taa inaweza kutumika kwa siku 108 na mafuta ya Ndege ya siku 35 ikiwa ni zaidi ya wastani wa kidunia wa siku 15.

“Tusijione kama tupo kwenye hali Mbaya, bali ni mwenendo wa Dunia nzima, tumetoka kwenye changamoto za UVIKO 19, na Sasa Vita ya Urusi na Ukraine imesababisha adha kubwa kwenye sekta ya nishati ya mafuta ikizingatiwa kuwa Urusi ni mzalishaji mkubwa wa nishati hiyo duniani” Mhandisi Godfrey Chibulunje – Kaimu Mkurugenzi Ewura.

#StarTvUpdate

The post Wakati Mataifa mbalimbali duniani yakiingia kwenye changamoto ya upatikanaji wa nishati ya mafuta na mfumuko wa Bei wa nishati h… appeared first on soka letu.



source https://mjombazecoder.website/3308/

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT