Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji Ewura, jumanne ijayo April 05 itatangaza Bei mpya ya nishati ya mafuta ikiwemo Petrol, Di…
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji Ewura, jumanne ijayo April 05 itatangaza Bei mpya ya nishati ya mafuta ikiwemo Petrol, Diesel, Mafuta ya Taa na Ndege ambayo inatajwa itakuwa juu zaidi kutokana na uhaba katika upatikanaji wa nishati hiyo kunakotokana na Vita ya Urusi na Ukraine.
Akizungumza Jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Ewura Mhandisi Godfrey Chibulunje, amewaasa Watanzania kukubaliana na hali hiyo kwani kupanda kwa Bei ya nishati ya mafuta si Tanzania pekee Bali kote duniani kumekumbwa na changamoto hiyo.
Hata hivyo amesema April 24 Mwaka huu, kuna meli zitaingiza mafuta nchini kupitia bandari ya Dar es salaam, Tanga na Mtwara huku mengine yakitarajiwa kuingizwa nchini Mwezi ujao kupitia Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa wote PBPA.
#StarTvUpdate

The post Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji Ewura, jumanne ijayo April 05 itatangaza Bei mpya ya nishati ya mafuta ikiwemo Petrol, Di… appeared first on soka letu.
source https://mjombazecoder.website/3306/
Comments
Post a Comment