Skip to main content
Na mwisho ni tabia ya kuendesha baiskeli kwa muda mrefu (kwa kipindi kimoja) ambayo hugandamiza neva na mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume na kusababisha mtu kupungukiwa na uwezo wa kusimamisha kwa muda na hatimaye kupungukiwa hamu ya kujamiana.
Vipimo vya uchunguzi
Ili kuweza kutambua chanzo cha tatizo hili, daktari huchukua historia ya maisha ya mhusika kwa ujumla, historia yake inayohusisha matumizi ya dawa aina mbalimbali, historia yake ya maisha ya ngono (sexual history) pamoja na kuchunguza dalili za magonjwa mbalimbali. Historia ya mgonjwa husaidia sana katika kufahamu ni vipimo na uchunguzi gani ufanyike. Vipimo hivyo vinaweza kuwa
  • Vaginal swab kwa ajili ya kuchunguza magonjwa ya zinaa au magonjwa mengine sehemu za siri za mwanamke
  • Uchunguzi wa mkojo (urinalysis)
  • Uchunguzi wa uwepo wa mabadiliko sehemu za siri za mwanamke kama vile mabadiliko ya kimaumbile (physical changes) kusinyaa kwa njia (thinning of genital tissues) kuwepo kwa makovu (scarring) na kupungua kwa hali ya kuvutika na ulaini wa ngozi ya sehemu hizo (decreased skin elasticity)
  • Kumpima akili mhusika
  • Kuchunguza kiwango cha homoni mbalimbali kama vile T3, T4 (kutoka tezi ya thyroid), testosterone (kutoka kwenye korodani), homoni ya ukuaji na homoni ya prolactin.
  • Uchunguzi wa shahawa (semen analysis) ambayo hujumuisha kuchunguza wingi wake (volume), kiwango chake (sperm count), mvutano wake (liquefaction time), maumbile ya mbegu (sperm morphology), pH yake, uwezo wa mbegu kuogelea (sperm motility), kiwango cha sukari na chembechembe nyeupe za damu.
  • Uchunguzi iwapo mhusika ana uzito unaolingana na urefu wake (body mass index, BMI) kulingana na umri wake
  • Vipimo vya ugonjwa wa shinikizo la damu hususani kwa wale wenye ugonjwa huo au wenye dalili zake au wale wanaotumia dawa za shinikizo la damu
  • Vipimo vya ugonjwa wa kisukari kama vile fasting blood glucose test (FBG), Oral Glucose Tolerance Test (OGTT), na glycosylated hemoglobin (Hb A1C).

Comments

Popular posts from this blog

Dr. William Samoei Ruto: muuza kuku ambaye sasa ni rais wa Kenya

Ruto ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza wa urais katika Jamhuri ya Kenya kushinda kura za urais katika jaribio la kwanza. Amekuwa naibu wa kwanza wa rais kushinda kiti cha urais katika Jamhuri ya Kenya. Mwanasiasa ambaye hajawahi kushindwa katika uchaguzi wowote. Mwanasiasa ambaye ametajwa na wachambuzi kama mchapa kazi na mwenye bidii na kiu ya kupata kile anacholenga maishani. Mtu asiyekata tamaa. Mcheshi katika hotuba zake, anayesemekana kutaka kujua kila linaloendelea karibu naye, mtu mkarimu mwenye roho ya kuchangisha pesa kwa watu na kwa ajili ya miradi mbalimbali. Ruto ameshutumiwa kwa kashfa kadhaa hasa za ufisadi bila kesi kufikishwa mahakamani, na ameshinda karibu kesi zote ambazo zimewahi kufunguliwa mahakamani dhidi yake ikiwemo kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Yafuatayo ndiyo mambo muhimu yanayomhusu rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoei Ruto. Majina Kamili: William Samoei Arap Ruto Umri: miaka 55 Mke wake: Rachel Chebet Ruto ...

Jioni

Download Audio The post Jioni appeared first on soka letu . source https://mjombazecoder.website/54168/

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye

Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kufuatia upigaji kura uliofanyika Jumapili mjini Mogadishu. Upigaji kura huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu uliokuwa na ulinzi mkali huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakilinda hema la Afisyone ambalo lilikuwa ni sehemu ya kupigia kura. Katika kikao cha pamoja cha mabaraza mawili ya bunge yenye wajumbe 328 waliwapigia kura wagombea 36 wa urais katika duru tatu. Mohamud alimshinda Rais aliyekuwa madarakani Mohammed Abdullahi Mohamnmed maarufu kama “Farmaajo” katika duru tatu za upigaji kura. Hassan Sheikh Mohamud alikuwa rais kati ya Agosti 2012 na Februari 2017. The post Bunge la Somalia limemchagua tena Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais ajaye appeared first on soka letu . Via soka letu https://ift.tt/ZmsWCwT