Je, tatizo hili linatibika?
Ndiyo! Habari njema ni kwamba tatizo la kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi linatibika kabisa. Jambo la muhimu ni kufahamu chanzo chake na kukishughulikia. Tiba inaweza kuhusisha mambo kama
- Kubadilisha mfumo wa maisha
- Kufanya mazoezi mara kwa mara husaidia kuongeza stamina, hupunguza uzito, kumfanya mtu kuwa na umbile zuri, furaha na kuongeza ufanisi wakati wa kujamiana
- Kupunguza msongo wa mawazo kwa kukubali kwamba lipo tatizo baina ya wenza na hivyo kutafuta suluhu pamoja na kuacha ugomvi. Fahamu kwamba malumbano na matatizo ni vitu vya kawaida katika uhusiano wowote. Ni vizuri kwa wenza kukaa pamoja na kuzungumza matatizo yao, kuwa wakweli, waaminifu na kuaminiana, kujaliana na kuzungumza juu ya tendo la ndoa kwa pamoja. Ni vizuri kila mmoja kuainisha vitu anavyopenda na asivyopenda kufanyiwa wakati wa kujamiana. Pale inapotokea mmoja hajapendezwa au kufurahishiwa na uwajibikaji au ufanisi wa mwenzake hana budi kutumia lugha nzuri kutafuta kiini cha tatizo na kulitafutia ufumbuzi.
- Pia matatizo ya kimaisha (fedha, nk) hayana budi kuzungumzwa kwa pamoja baina ya wenza na kisha kutafutiwa ufumbuzi
- Kufanya mazoezi ya misuli ya nyonga (pelvic muscles) kwa kufanya kama unazuia mkojo wakati unahisi haja ndogo na kuhesabu moja hadi tano, baada ya tano pumzika na halafu rudia tena. Mazoezi ya namna hii (Kegel’s exercise) huongeza uwezo wa kujamiana kwa wanawake.
- Weka mazingira mazuri na muda wa kufanya tendo la ndoa na mwenza wako ili mpate kudumisha uhusiano wenu
- Ongeza msisimko katika uhusiano wenu kwa kujaribu aina, mbinu na mikao mbalimbali wakati wa kujamiana, kubadili muda wa kufanya mapenzi (si
Comments
Post a Comment